TAHA-Report on the effect of COVID-19 to the Horticulture Industry

Download this Report

 

TAARIFA YA ATHARI YA HOMA YA VIRUSI VYA CORONA KATIKA TASNIA YA HORTICULTURE NCHINI TANZANIA

 1. UTANGULIZI

Tasnia ya horticulture nchini Tanzania (uzalishaji na uuzaji wa maua, mboga, matunda, viungo, mbegu na mazao ya mizizi –viazi) ni mojawapo ya tasnia inayokuwa kwa kasi zaidi, ikikua kwa wastani wa asilimia kumi na moja (11%) kwa mwaka. Tasnia hii pia ni mchangiaji mkubwa wa mapato ya kigeni katika sekta ya kilimo, ikichangia wastani wa asilimia arobaini na tatu (43%). Tasnia ya horticulture pia imeajiri zaidi ya watu milioni nne (4,000,000) wengi wakiwa wanawake na vijana. Mbali na mchango wa kiuchumi, tasnia hii inachangia kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji wa lishe bora na usalama wa chakula nchini.

 

Mazao mengi ya horticulture yanayozalishwa nchini yanauzwa katika masoko ya kikanda na kimataifa. Sehemu kubwa ya mazao yanayouzwa kwenye masoko haya yanazalishwa na wazalishaji wakubwa na baadhi ya uzalishaji unafanywa wazalishaji wadogo ‘out growers’ wenye mikataba ya uzalishaji na wazalishaji wakubwa.

 

Kutokana na changamoto ya kuenea kwa homa ya virusi vya Korona duniani na hasa katika nchi za bara la Ulaya, Amerika na Asia, mahitaji ya bidhaa za mazao ya horticulture hususan mazao ya jamii ya maua katika nchi hizo yameshuka kwa zaidi ya asilimia hamsini (50%) na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa wazalishaji wa mazao hayo hapa nchini wanaouza mazao yao katika masoko ya kimataifa.

 

 1. ATHARI KWA TASNIA YA HORTICULTURE

 

 1. UZALISHAJI

Kutokana na kuporomoka kwa masoko ya kimataifa ya mazao ya horticulture, wanunuzi wengi wa kimataifa wamesitisha kununua mazao hayo na hivyo kupelekea changamoto kubwa kwa upande wa wazalishaji wa mazao haya hapa nchini. Mauzo ya wazalishaji wengi yameshuka kwa zaidi ya asilimia hamsini (50%) ndani ya kipindi kifupi tangu kuanza kuenea kwa ugonjwa huu.

 

Mengi ya mazao haya yanayouzwa katika masoko ya kimataifa, yana uhitaji mdogo sana na mengine hayana uhitaji kabisa katika masoko ya ndani hivyo wazalishaji wa mazao haya hawana masoko mbadala ya kupeleka bidhaa zao zaidi ya kuendelea kuzihifadhi kwa muda mfupi na baadaye kuziteketeza kabisa.

 

Kutokana na changamoto hii, wawekezaji wengi wapo katika hali ya sintofahamu kwa kuwa licha ya kuwa hawawezi kuuza bidhaa wanazozalisha lakini wanaendelea kuingia gharama za uendeshaji wa mashamba yao ikiwemo mishahara ya wafanyakazi n.k. Kwa kuwa hali hii inadhaniwa kuendelea kwa kipindi ambach bado hakijulikani, baadhi ya wawekezaji wanafikiria kusimamisha ajira za wafanyakazi kwa kipindi kisichojulikana na wengine wanafikiria kufunga mashamba yao

 

 1. USAFIRISHAJI

Ndege nyingi za abiria ambazo pia hubeba bidhaa za mboga, maua na matunda zimepunguza na nyingine kusitisha kabisa safari zake katika maeneo mbalimbali duniani. Kadhia hii imeathiri kwa kiasi kikubwa uuzwaji wa mazao ya horticulture kutoka Tanzania kwenda kwenye masoko ya kimataifa. Kutokana na changamoto hii, upatikanaji wa nafasi za mizigo katika ndege zinazokwenda kwenye masoko ya nje ya nchi (Ulaya, Amerika, Asia na Mashariki ya Kati) umeathirika kwa asilimia mia moja (100%). Upungufu huu wa nafasi umeathiri kwa kiasi kikubwa uuzwaji wa mazao ya horticulture kutoka Tanzania kwenda kwenye masoko ya kimataifa.

 

Kwa wastani, mazao ya horticulture yenye thamani ya Dola za Kimarekani 63,684,799 husafirishwa kila mwezi kutoka Tanzania kwenda katika masoko ya kimataifa. Kutokana na athari zitokanazo na mlipuko wa homa ya Corona usafirishaji wa mazao haya umepungua kwa zaidi ya asilimia 80 na hivyo kuifanya nchi kupoteza mapato ya kigeni ya takribani Dola za Kimarekani 50,947,839 kwa mwezi.

 

 1. KUFUNGWA KWA MIPAKA YA NCHI JIRANI

Kutokana na upungufu huu wa ndege zinazokuja Tanzania, wazalishaji wengi wameamua kutumia njia mbadala kwa kusafirisha mazao yao kupitia viwanja vya ndege vya nchi jirani ili kuweza kufikisha bidhaa zao katika masoko ya kimataifa. Njia hii mbadala imekuwa ikikumbwa na changamoto za mara kwa mara kutokana na mipaka ya nchi ya Kenya kufungwa kwa vipindi tofauti ili kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa huu

 

 1. KUPOROMOKA KWA MASOKO YA NJE

Kutokana na kuporomoka kwa masoko ya kimataifa ya mazao ya horticulture, wanunuzi wengi wa kimataifa wamesitisha kununua mazao hayo na hivyo kupelekea changamoto kubwa kwa upande wa wazalishaji wa mazao haya hapa nchini. Mauzo ya wazalishaji wengi yameshuka kwa zaidi ya asilimia hamsini (50%) ndani ya kipindi kifupi tangu kuanza kuenea kwa ugonjwa huu.

 

Mengi ya mazao haya yanayouzwa katika masoko ya kimataifa, yana uhitaji mdogo sana na mengine hayana uhitaji kabisa katika masoko ya ndani hivyo wazalishaji wa mazao haya hawana masoko mbadala ya kupeleka bidhaa zao zaidi ya kuendelea kuzihifadhi kwa muda mfupi na baadaye kuziteketeza kabisa.

 

 1. AJIRA

Shughuli nyingi katika tasnia ya horticulture zinatumia wafanyakazi wengi zaidi kuliko mashine ‘labor intensive’ hasa katika uvunaji, uchambuaji, upangaji wa madaraja na ufungushaji. Hii imepelekea mashamba mengi makubwa kuajiri idadi kubwa ya wafanyakazi.

 

Kutokana na changamoto hii, waajiri wengi wanafikiria kupunguza zaidi ya asilimia themanini (80%) ya wafanyakazi ili kupunguza gharama za uendeshaji katika kipindi hiki ambapo hakuna mauzo. Punguzo hili la wafanyakazi litasababisha kupotea kwa zaidi ya ajira 6,000 za moja kwa moja na hivyo kuleta madhara makubwa ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa. Kusimama kwa shuguli za uzalishaji katika mashamba haya utaathiri pia makampuni lukuki yanatoa huduma na kuuza bidhaa mbalimbali (pembejeo, zana, teknolojia, vifungashio n.k) katika mashamba haya

 

Pia wauzaji wengi wa mazao ya horticulture katika masoko ya kimataifa wameingia mikataba ya uzalishaji na wakulima wadogo (Out Growers) hivyo changamoto hii ya kuporomoka kwa masoko itawaathiri pia zaidi ya wakulima wadogo 15000.

 

 1. UPATIKANAJI WA PEMBEJEO NA TEKNOLOJIA

Mlipuko wa corona kwa kiasi fulani umeanza kuathiri upatikanaji wa pembejeo kama mbolea na madawa. Tanzania inategemea kuagiza kutoka nje zaidi ya asilimia 90 ya pembejeo na teknolojia za horticulture hivyo mabadiliko yoyote ya uzalishaji wa vitu hivyo yataathiri sekta ya horticulture kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, nchini China, zaidi ya asilimia 50 ya viwanda vya mbolea vimesitisha kuzalisha. Vivyovivyo barani Ulaya, viwanda vimeanza kupunguza uzalishaji.

 

Kwa sababu hiyo basi, changamoto hii ikiendelea kwa muda mrefu zaidi kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa uhaba wa pembejeo na hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao hasa ya horticulture na hivyo kuathiri wakulima zaidi ya milioni nne.

 

 1. MAPENDEKEZO

Kutokana na kadhia hii, BARAZA linapendekeza hatua zifuatazo kuchukuliwa ili kuinusuru tasnia za horticulture, pamoja na sekta nyingine zilizoathirika zaidi kama uvuvi, kuku, nafaka na mikunde, tumbaku na kahawa:

 • Serikali iangalie uwezekano wa kutoa fidia (stimulus) katika tasnia hizi kama ilivyofanya kwenye tasnia ya pamba wakati wa mdororo wa uchumi duniani.
 • Serikali kupitia Benki Kuu itoe ruhusa maalumu kwa benki za biashara kulegeza baadhi ya masharti ya mikopo (marejesho) kwa kipindi hiki mpaka hapo hali itakapokuwa nzuri kibiashara Tunapendekeza ruhusa na utaratibu huu utumike kwa yale makampuni yatakawasilisha maombi kwa taasisi za fedha husika.
 • Serikali iwe na makubaliano na nchi jirani na mataifa mengine ili kuruhusu biashara ya bidhaa za Tanzania kufanyika huku ikiimarisha usalama wa afya za walaji. Hata kama italazimika kufungwa kwa mipaka basi kuwe na makubaliano ya nchi kwa nchi ya kuruhusu mizigo kuingia (cargo) na hasa pia usafirishaji wa mazao na pembejeo za kilimo.
 • Serikali iangalie uwezekano wa kutoa msamaha maalumu kwa waajiri kutolipa kodi na tozo nyingine zinazohusiana na ajira kwa kipindi maalum ili kunusuru upotevu wa ajira za wafanyakazi.
 • Kupitia taasisi na vyombo mbalimbali vya serikali, serikali iwaandae wakulima na wadau wengine kuhusu uwezekano wa anguko la bei na kupanda kwa pembejeo kutokana na ugonjwa wa korona ili suala hili lisije leta mtafaruku hasa wakati wa msimu wa masoko masoko kwa mazo kama Korosho, pamba na Mengineyo.

 

Download this Report